Saturday, September 7, 2013
KIUFUNDI ZAIDI: KWANINI ROBIN VAN PERSIE HAJAPIGA HATA SHUTI MOJA GOLINI KATIKA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL NA CHELSEA?
Robin van Persie alikuwa kwenye kiwango kizuri dhidi ya Swansea katika mchezo wa ufunguzi wa msimu. Mshambuliaji huyo wa kidachi alionekana ameuanza msimu kama alivyoumaliza uliopita akiwa kwenye fomu nzuri. Pamoja na kufunga mabao mawili katika mechi ya kwanza, van Persie ameshindwa kupiga hata shuti moja lilolenga goli katika michezo miwili iliyopita - mechi ambazo Manchester United ilifeli kufunga bao hata moja.
Kiwango cha van Persie kwa ujumla katika mechi mbili zilizopita.
Okay! kama tulivyoona kwamba RVP hakupiga mpira wowote uliolenga goli huku wastani wake wa kupiga mipira ukipungua mpaka 33%. Dhidi ya Liverpool,mambo yakawa mabaya zaidi huku akipoteza nafasi mbili kwa kupiga mipira nje huku jaribio lake la 3 likizuiwa na walinzi wa lango la Liverpool.
Sio tu kwamba alionekana kutokuwa mchezoni pia alikosa ideas kabisa mbele ya lango (kwa ubora wake) lakini pia mchango wake kwenye umekuwa wa chini sana. Namba ya pasi kwa mchezo imekuwa ikipungua vibaya sana tangu siku ya mchezo wa kwanza, kama ilivyo wastani wake wa usahihi wa pasi:Dhidi ya Liverpool huu ulikuwa ushahidi kwamba mdachi huyo alipiga pasi sahihi 13 tu sahihi ukilinganisha na pasi 27 kwa mchezo msimu uliopita. Katika pasi hizi zote hakukuwa hata na moja ya kupenyeza na katika katika pasi zilizofika 9 zilikuwa za kurudi nyuma katika safu ya kiungo, tofauti tulivyomzoea mdachi huyo ambaye alitengeneza nafasi 71 kwa wachezaji wenzie msimu uliopita. Mwaka huu anaonekana kushindwa kufikia aliyoyafanya msimu uliopita, akitengeneza nafasi moja tu katika mechi tatu. Hiyo nafasi moja ilikuja kwenye mchezo dhidi ya Swansea, hivyo kufanya mchango wake katika mechi mbili kuwa zero kabisa.
Nini tatizo?
Ni sawa sasa hivi ni mapema sana kupaniki, lakini ni vizuri kugundua udhaifu. Van Persie alikaukiwa kama hivi msimu uliopita, hivyo ni suala la kuliangalia kwa umakini kwa United. Katika kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool van Persie alikuwa mpweke sana mbele kwa mara kadhaa, akikosa huduma muhimu kama ilivyozoeleka.
Huku Wayne Rooney akiwa hachezi katika mchezo dhidi ya Liverpool Danny Welbeck alipewa jukumu la kucheza pembeni ya RVP - kumsaidia na kumpa huduma huduma muhimu mdachi huyo. . Welbeck, ni mzuri katika kumiliki mpira, lakini hana uwezo mzuri wa kuingiza mipira ndani na ilivyo kwa RVP nae alitengeneza nafasi moja tu msimu huu, katika sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea, akifeli kabisa kuiunganisha timu dhidi ya Liverpool. Rooney, ambaye alicheza kidogo katika mechi dhidi ya Swansea na dhidi ya Chelsea tayari ametengeneza nafasi 3 jambo ambalo linaonyesha tofauti anayoweza kuleta kwenye timu anapokuwa anacheza.
Dhidi ya Liverpool ingawa ilikuwa 4-4-2, huku Welbeck akicheza karibu sana na van Persie kitu ambacho kilikuwa kizuizi kucheza kwa kubadilishana, kwa kawaida Rooney huingia kati ya mistari na kuchukua mpira kutoka kwenye kiungo na baada ya hapo kumtengenezea RVP katika njia nyuma yake, au kumpenyezea mpira kwa mbele: RVP (20) yupo karibu sana na Welbeck (19) na huku wachezaji walioanza inaonekana ni 4-4-2 zaidi. Msimu uliopita mfumo ulikuwa tofauti na huu, huku mfumo wa 4-4-2 ukiwa hatumiki saa na makocha wa kisasa. Mfumo huu unatajwa kutengeneza nafasi chache sana kwa Manchester United, ambao wametengeneza wastani wa nafasi 8 tu kwa mchezo msimu huu, ukilinganisha na namba kubwa ya msimu uliopita wastani wa 11.5 kwa mchezo. Hivyo, kesi inaweza kuwa kwamba United haina ubunifu hivi sasa. Katika michezo miwili iliyopita United ilitengeneza nafasi 7 tu - hii ni rekodi mbovu kabisa katika historia ya hivi karibuni ya timu hiyo.
Kukosekana kwa Rooney’ kunasababisha hili, huku mshambuliaji huyo wa England akitengeneza 12%ya jumla ya nafasi zote walizotengeneza United msimu huu, pamoja na kucheza pungufu ya dakika 150. Inawezekana ikawa jambo la busara sasa kwa Moyes kuanza kumtumia Shinji Kagawa nyuma ya RVP katika michezo ambayo Rooney hachezi. Kagawa anaweza kucheza katikati ya mistari na kuinganish timu kati safu ya kiungo na ushambuliaji kwa ubora mkubwa kuliko afanyavyo Danny Welbeck. Kagawa ingawa inaonekana kama hana nafasi kubwa sana kwa kocha mpya David Moyes.
Hitimisho
Ingawa ni mapema sana mwa msimu lakini kumekuwa na wasiwasi wa namna United wanavyokosa ubunifu katika kulishambulia lango hasa katika michezo miwili mikubwa iliyopita - ambayo tumeshuhudia mshambuliaji wao tegemeo akishindwa hata kupiga shuti moja akilenga goli. Kumuingiza Kagawa katika timu kunaweza kusaidia kutibu ugonjwa unaisumbua timu hasa katika wakati huu mtu ambaye huifanya kazi kwa ufanisi Wayne Rooney akiwa nje ya dimba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment