Saturday, September 7, 2013

BUNGENI KIDOGO

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi (SUGU) akitolewa kwa nguvu nje ya Ukumbi wa Bunge jana akipinga kitendo cha Askari wa Bunge kumtoa nje Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe baada ya Naibu Spika Job Ndugai kutoa amri hiyo.
PICHA ZAIDI & VIDEO =>

Azam TV kama Ulaya Muda si mrefu itakuwa Hewani

Kamera hizi ni ghali zikiwa zimegharimu kiasi cha kuanzia dola 180,000 hadi dola 200,000 kwa kila moja POPOTE utakapotulia na kutazama pambano lolote litakaloonyeshwa moja kwa moja au kwa marudio, kupitia kituo cha Televisheni cha Azam (Azam TV), usiwe na shaka, utaliona pambano maridadi. Weka soda yako sebuleni kando kisha watazame Jerry Santo na Amri Kiemba wakichuana katikati ya uwanja wowote ule wa soka nchini huku kamera nane za Azam TV zinazorekodi pambano lao zikiwachukua kwa umaridadi. Kamera nane zamrekodi mchezaji Katika pambano lolote litakaloonyeshwa na Azam TV kutakuwa na kamera nane uwanjani. Huu ni wastani wa juu wa idadi ya kamera zinazopaswa kuonyesha kwa ufasaha pambano lolote la soka ingawa katika mechi za ligi nyingine au michuano mingine kunakuwa na kamera zaidi za kuonyesha mbwembwe mbalimbali. Kamera hizi ni ghali zikiwa zimegharimu kiasi cha kuanzia dola 180,000 hadi dola 200,000 kwa kila moja. Ndani ya kila kamera kuna mchanganyiko wa mashine ya Sony huku lensi ya kuvutia matukio kwa ufasaha ikiwa ni ya kampuni ya Cannon. Kamera mbili zitakuwa zinakaa katika kila nyuma ya lango la uwanja. Kamera hizi mbili zina kishikilio kirefu na kuifanya ining’inie katika eneo lote la nyuma ya lango kama tunavyoona katika mechi za Ligi Kuu England na michuano mbalimbali. Katika pande mbili za uwanja, karibu na benchi la kila timu kutakuwa na kamera mbili ambazo watu wanaorekodi mpira wataweza kukimbia nazo huku na kule kwa ajili ya kutokana matukio yanayoendelea katika upande wa kulia na kushoto kuanzia pale anapokaa mwamuzi wa akiba. Kamera ya nne ni ile iliyosimama katikati ya uwanja, karibu na mwamuzi wa akiba. Kamera hiyo huwa inasimama ilipo na haisogei. Dhumuni kubwa ni kuzivuta kwa karibu sura za wachezaji au mwamuzi inapohitajika. Jukwaani kuna kamera kubwa zaidi, pengine kuliko zote. Mtambo huu unarekodi mechi yote kwa juu na ni nzuri kwa mwelekeo mzima wa ‘muvu’ kwa timu zote mbili. Lakini pia kando ya kamera hii kuna kamera nyingine kubwa ambayo nayo inadaka kwa haraka matukio ya ndani ya uwanja. Pia bado kuna kamera ya saba ya mtu ambaye anazunguka katika kando ya uwanja kwa ajili ya kuchukua mahojiano kabla ya mechi, wakati wa mapumziko na mechi ikiisha. Kamera zote hizi saba zina uwezo wa kurekodi na kuvuta kwa karibu tukio lililo umbali wa mita 400 kutoka zilipo. Hii ni sawa na muunganiko wa viwanja vinne vya mpira! OB Van ya kisasa zaidi barani Ulaya Kamera hazina kazi yoyote kama huna OB (Outside Broadcasting)Van ya kisasa. OB Van ni gari linalokamata matangazo uwanjani na kwingineko nje ya studio kutokea katika kamera na kurusha katika setalaiti iliyo hewani. OB Van ya Azam TV ni ya kisasa zaidi ambayo ni zaidi ya OB Van zinazotumiwa na kampuni nyingine za Afrika. Ikiwa imegharimu kiasi cha Euro 4 milioni, OB Van hiyo ililetwa nchini na Kampuni ya Broadcast Solutions ya Ujerumani chini ya mhandisi wake maarufu, Armando Santos ambaye ameondoka nchini jana Ijumaa baada ya kuendesha mafunzo maalumu ya jinsi ya kuitumia OB Van hiyo.

Wanafunzi walipukiwa na bomu morogoro wakidhani ni Bulbu.

Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari matombo katika wilaya ya morogoro wamejeruhiwa, na wengine watatu kunusurika, baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu, wakati wakitoka shuleni. Wanafunzi hao waliojeruhiwa katika sehemu mbalimbali za miili yao ni Luciani Juma (14) na Anthonia Charles (15), wakazi wa kijiji cha Konde, Tarafa ya Matombo wilayani Morogoro, ambapo Luciani aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu, ameiambia itv kuwa walipatwa na tukio hilo wakati wakitokea shuleni, ambapo njiani walikutana na kitu mfano wa balbu ya tochi ambacho hata asubuhi wakati wa kwenda shule walikiona na kukipuuza, na mmoja wawanafunzi alikirushia ganda la muwa aliokuwa akila, na kililipuka na kutoa mshindo mkubwa. Daktari anayemtibu Lucien katika wadi namba moja ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, aliyejulikana kwa jina moja Dk. Francis amesema majeruhi huyo anaendelea vizuri, na amepata majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo sehemu za siri, kwenye paja na sehemu ya nyonga na kwamba katika maeneo hayo walifanikiwa kutoa vitu mfano wa chuma.

HUYU NI BINTI WA KIDATO CHA NNE INASEMEKANA AMEZAA NA DIAMOND PLATNUMZ..!! ETI NI KWELI HUYU MTOTO KAFANANA NA DIAMOND??!!

MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. MCHEZO MZIMA Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano. Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo. Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo. Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.
WAKUTANA Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’. Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa. WEMA ATAJWA Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo. Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu. Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani. Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna. ‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’. Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia. Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana. Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya na walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa. Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao. Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina. SASHA AKIRI Baada ya kupata madai hayo,tulimsaka Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena, naye aliacha kumfuatilia. “Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha. HUYU HAPA DIAMOND Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya kiganjani akiwa Nairobi, Kenya na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya ishu hiyo, alieleza: “Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.” Katika kuonesha ‘usiriazi’, tuliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha

KIUFUNDI ZAIDI: KWANINI ROBIN VAN PERSIE HAJAPIGA HATA SHUTI MOJA GOLINI KATIKA MECHI DHIDI YA LIVERPOOL NA CHELSEA?

Robin van Persie alikuwa kwenye kiwango kizuri dhidi ya Swansea katika mchezo wa ufunguzi wa msimu. Mshambuliaji huyo wa kidachi alionekana ameuanza msimu kama alivyoumaliza uliopita akiwa kwenye fomu nzuri. Pamoja na kufunga mabao mawili katika mechi ya kwanza, van Persie ameshindwa kupiga hata shuti moja lilolenga goli katika michezo miwili iliyopita - mechi ambazo Manchester United ilifeli kufunga bao hata moja. Kiwango cha van Persie kwa ujumla katika mechi mbili zilizopita. Okay! kama tulivyoona kwamba RVP hakupiga mpira wowote uliolenga goli huku wastani wake wa kupiga mipira ukipungua mpaka 33%. Dhidi ya Liverpool,mambo yakawa mabaya zaidi huku akipoteza nafasi mbili kwa kupiga mipira nje huku jaribio lake la 3 likizuiwa na walinzi wa lango la Liverpool. Sio tu kwamba alionekana kutokuwa mchezoni pia alikosa ideas kabisa mbele ya lango (kwa ubora wake) lakini pia mchango wake kwenye umekuwa wa chini sana. Namba ya pasi kwa mchezo imekuwa ikipungua vibaya sana tangu siku ya mchezo wa kwanza, kama ilivyo wastani wake wa usahihi wa pasi:Dhidi ya Liverpool huu ulikuwa ushahidi kwamba mdachi huyo alipiga pasi sahihi 13 tu sahihi ukilinganisha na pasi 27 kwa mchezo msimu uliopita. Katika pasi hizi zote hakukuwa hata na moja ya kupenyeza na katika katika pasi zilizofika 9 zilikuwa za kurudi nyuma katika safu ya kiungo, tofauti tulivyomzoea mdachi huyo ambaye alitengeneza nafasi 71 kwa wachezaji wenzie msimu uliopita. Mwaka huu anaonekana kushindwa kufikia aliyoyafanya msimu uliopita, akitengeneza nafasi moja tu katika mechi tatu. Hiyo nafasi moja ilikuja kwenye mchezo dhidi ya Swansea, hivyo kufanya mchango wake katika mechi mbili kuwa zero kabisa. Nini tatizo? Ni sawa sasa hivi ni mapema sana kupaniki, lakini ni vizuri kugundua udhaifu. Van Persie alikaukiwa kama hivi msimu uliopita, hivyo ni suala la kuliangalia kwa umakini kwa United. Katika kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool van Persie alikuwa mpweke sana mbele kwa mara kadhaa, akikosa huduma muhimu kama ilivyozoeleka. Huku Wayne Rooney akiwa hachezi katika mchezo dhidi ya Liverpool Danny Welbeck alipewa jukumu la kucheza pembeni ya RVP - kumsaidia na kumpa huduma huduma muhimu mdachi huyo. . Welbeck, ni mzuri katika kumiliki mpira, lakini hana uwezo mzuri wa kuingiza mipira ndani na ilivyo kwa RVP nae alitengeneza nafasi moja tu msimu huu, katika sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea, akifeli kabisa kuiunganisha timu dhidi ya Liverpool. Rooney, ambaye alicheza kidogo katika mechi dhidi ya Swansea na dhidi ya Chelsea tayari ametengeneza nafasi 3 jambo ambalo linaonyesha tofauti anayoweza kuleta kwenye timu anapokuwa anacheza. Dhidi ya Liverpool ingawa ilikuwa 4-4-2, huku Welbeck akicheza karibu sana na van Persie kitu ambacho kilikuwa kizuizi kucheza kwa kubadilishana, kwa kawaida Rooney huingia kati ya mistari na kuchukua mpira kutoka kwenye kiungo na baada ya hapo kumtengenezea RVP katika njia nyuma yake, au kumpenyezea mpira kwa mbele:
RVP (20) yupo karibu sana na Welbeck (19) na huku wachezaji walioanza inaonekana ni 4-4-2 zaidi. Msimu uliopita mfumo ulikuwa tofauti na huu, huku mfumo wa 4-4-2 ukiwa hatumiki saa na makocha wa kisasa. Mfumo huu unatajwa kutengeneza nafasi chache sana kwa Manchester United, ambao wametengeneza wastani wa nafasi 8 tu kwa mchezo msimu huu, ukilinganisha na namba kubwa ya msimu uliopita wastani wa 11.5 kwa mchezo. Hivyo, kesi inaweza kuwa kwamba United haina ubunifu hivi sasa. Katika michezo miwili iliyopita United ilitengeneza nafasi 7 tu - hii ni rekodi mbovu kabisa katika historia ya hivi karibuni ya timu hiyo. Kukosekana kwa Rooney’ kunasababisha hili, huku mshambuliaji huyo wa England akitengeneza 12%ya jumla ya nafasi zote walizotengeneza United msimu huu, pamoja na kucheza pungufu ya dakika 150. Inawezekana ikawa jambo la busara sasa kwa Moyes kuanza kumtumia Shinji Kagawa nyuma ya RVP katika michezo ambayo Rooney hachezi. Kagawa anaweza kucheza katikati ya mistari na kuinganish timu kati safu ya kiungo na ushambuliaji kwa ubora mkubwa kuliko afanyavyo Danny Welbeck. Kagawa ingawa inaonekana kama hana nafasi kubwa sana kwa kocha mpya David Moyes. Hitimisho Ingawa ni mapema sana mwa msimu lakini kumekuwa na wasiwasi wa namna United wanavyokosa ubunifu katika kulishambulia lango hasa katika michezo miwili mikubwa iliyopita - ambayo tumeshuhudia mshambuliaji wao tegemeo akishindwa hata kupiga shuti moja akilenga goli. Kumuingiza Kagawa katika timu kunaweza kusaidia kutibu ugonjwa unaisumbua timu hasa katika wakati huu mtu ambaye huifanya kazi kwa ufanisi Wayne Rooney akiwa nje ya dimba.

WAPINZANI WAKATAA KUUNGA MKONO MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA KATIBA YA MWAKA 2013

Kambi ya upinzani bungeni imesema kutokana na mtafuruku uliotokea bungeni kwa kutolewa nje kiongozi wa kambi hiyo Mh. Freeman Mbowe amesema hawaungi mkono muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2013 kwa kuwa haiwatendei haki watanzania. Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni mjini Dodoma kuhusiana na mtafuruku uliotokea bungeni kiongozi huyo wa kambi ya upinzai bungeni Mh Freeman Mbowe amesema hawatashiriki katika mjadala huo kwa kile walichodai kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kina ajenda ya siri na kushiriki kwao hawatakuwa wanawatendea haki watanzania Akizungumzia juu ya kile kinachoonekana kwa sasa kuwa ni uhusiano mwema baina ya chama cha wananchi (CUF) na Chadema,mbunge wa Mkanyageni kupitia CUF Mh Habib Mnyaa amesema siasa haina adui wala rafiki wa kudumu na hivo wameungana na Chadema katika kutetea haki,usawa na maslahi ya wananchi wa Zanzibara na wale wa Tanzania Bara Katika tukio jingine wanasheria wa masuala ya haki za binadamu wamesema kilichotokea bungeni ni kutokana na kitendo cha naibu spika kuchelewa kutoa majibu ya miongozo kama ilivyoombwa na baadhi ya wabunge na kuwafanya wabunge wa upinzani kuona wanaburuzwa na kuamua kutoka nje na kuongeza kuwa hawakufurahishwa na jambo hilo kwa kile alichodai kuwa mawazo yawachache yanapigwa kumbo

Thursday, September 5, 2013

KIDONDA CHA AUNT EZEKIEL CHAOZA YUPO HATARINI KUKATWAMKONO..!!

INASIKITISHA! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na jeraha la chupa alilolipata hivi karibuni.
Tukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.
Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda.

ALIKATISHA DOZI
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.
Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.
“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.

ASAFISHWA UPYA
Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.
MKONO ULIANZA KUOZA
Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari, akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono.
 “Iligundulika mkono ulikuwa unaoza, daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema nesi huyo.
CHANZO CHA UGOMVI NI NINI?
Licha ya kuhusishwa na ugomvi wa kimapenzi baina yake na mpenzi wa Yvonne anayejulikana kwa jina la Joff, Aunt alisema ugomvi wao uliisha zamani na kila mmoja ana maisha yake.
“Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu,” alisema Aunt.
Wakati huohuo, taarifa ambazo Amani limezipata kuhusu mtuhumiwa wa Aunt, Yvonne ambaye alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar siku ya tukio, anahaha kukwepa kifungo kwani uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani kisha gerezani.